Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.Mtoto wa
marehemu, Benjamin Sitta amesema baba yake amefariki saa 10:00 usiku wa kuamkia
leo.‘’Nikweli mzee amefariki nchini Ujerumani akiwa anapatiwa matibabu,
alipelekwa Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbulia na saratani ya tezi dume
ambayo ilisambaa na kuathiri miguu na mwili mzima."Benjamin amesema
kuwa taarifa za mipango ya kusafirisha mwili zitatolewa baadaye.Sitta alikuwa
Spika wa Bunge tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2010 na pia mbunge wa Urambo
Mashariki.Pia, alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na aliwahi kuwa
waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti.Alikuwa miongoni mwa
wanachama zaidi ya 42 wa CCM waliochukua fomu za kugombea urais mwaka jana.
Posted by Elias Magugudi
Kurunzi za Siasa
eliasmagugudi2016@gmail.com
0 comments:
Post a Comment