Mkuu Mpya mteule wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Mrisho Gambo
Niungane wa wadu wengine wa siasa za Tanzania kumpongeza Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Mrisho Gambo. Umeonyesha juhudi kubwa katika utumishi wako ukiwa Mkuu wa Wilaya, natumaini ndio sababu kubwa iliyokupandisha hadi nafasi hio ya juu katika Mkoa. Kilichobadilika hapo ni eneo la utawala toka Wilaya na sasa Mkoa. Na kwa utendaji wako mimi naamini utaimudu nafasi hio bila shaka lolote.
Mkoa wa Arusha ni moja ya Mikoa yenye changamoto nyingi sana ambazo kama Mkuu wa Mkoa unatakiwa kuziishi na kuzifanya sehemu ya maisha yako. Mheshimwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameonyesha imani kubwa kwako hakikisha unadhibitisha ubora wako katika kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Arusha kwa ujumla wao bila kujali tofauti zao za kisiasa.
Napenda pia kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa vile uteuzi anaoufanya unatia moyo, kwamba kiongozi anatakiwa apande ngazi kutokana na juhudi zake, Na juhudi hizo zimeendelea kuonekana mfano mzuri ni uteuzi wa Mheshimiwa Paul Makonda ambaye tangu apandishe cheo anaendelea kufanya vizuri sana katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Dar es salam.
Natumaini Mheshiniwa Gambo, utaendelea kufanya vizuri, na utendaji wako utakua mkubwa zaidi maana umepewa jukumu la kuwahudumia wananchi wengi zaidi
Mwenyezi Mungu akusaidie katiak Utumishi wako kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
0 comments:
Post a Comment