BAADA
ya kutenguliwa kwake na Rais Dkt. John Magufuli, aliyekuwa Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, NIMR, Dr Mwele
Malechela, wakati huo Rais amemteua Prof. Yunus Daud Mgaya kujaza nafasi
hiyo.
Wakati kutenguliwa kwa Dkt. Mwele
kumekuja siku moja tu baada ya kuzungumza na waandishi na kudai kuwepo
kwa virusi vya Zika nchini. Alisema kati ya watu 533 waliopimwa wakati
wa utafiti walioufanya, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi
hivyo. Taarifa yake, ilikuja kukanushwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Mwanaharakati na Kiongozi wa Chama cha
ACT-Wazalendo, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Prof. Kitila Mkumbo amehoji uhalali wa wanasiasa kutangaza tafiti
zinazofanywa na watu wenye taaluma husika (wanasayansi).
Ujumbe huo wa Prof. Mkumbo umetafsriliwa
na baadhi ya watu kuwa huenda anahoji uhalali wa Waziri wa Afya, Ummy
Mwalim kukanusha taarifa za tafiti ilihali waliyoitoa taarifa hiyo
(NIMR) ndiyo wataalam haswa wa masuala ya tafiti.
Kupitia ukurasa wake akaunti yake ya mtandao wa Twitter, Prof. kitila Mkumbo ameandika haya.
0 comments:
Post a Comment