Wajumbe wa Mkutano Mkuu
wa CCM wakiwa katika moja ya mikutano mjini Dodoma.
Napenda
kutumia wasaa huu kuzungumzia mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Dodoma
July 23, 2016 ukiwa na lengo kuu la kumchagua Mwenyekiti mpya wa CCM.
Ni
ukweli usiokua na shaka kwamba Mkutano wa CCM unatazamwa na watu wengi kwa
sababu matokeo yake yatabeba matumaini mapya kwa wana CCM na Watanzania kwa
ujumla.
Nichukue
nafasi hii kumshukuru na kumpongeza Mwenyekiti anayestaafu Dr. Jakaya Kikwete
kwa sababu anakabidhi Chama Kikiwa salama na pia ametimiza malengo na madhumuni
ya CCM kwa mujibu wa Katiba ambayo kati ya malengo hayo ni haya yafuatayo;-
Ibara ya 5(1) na (2) inatamka kama ifuatavyo-
Kwa
hiyo malengo na madhumuni ya CCM yatakua kama yafuatayo-
(1)
Kushinda katika
Uchaguzi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa Tanzanai Bara na Zanzibar ili
kuunda na kushika Serikali Kuu na Serikali za mitaa katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
(2)
Kulinda na
kudumisha Uhuru wa Nchi yetu na raia wake.
Mheshimiwa
Kikwete ameyatekeleza haya pamoja na majukumu mengine kwa moyo wa dhati na kwa
uwezo wa Mungu anatukabidhi Chama kikiwa salaama ili Kiongozi mwingine aendelee
pale alipoishia. Dr. Jakaya Kikwete tunakushuru kwa utumishi wako mwema
ndani ya Chama na Selikalini kwa ujumla.
Siku
mbili zijazo CCM itakua na Mwenyekiti mpya ambaye sina shaka ni Dr. John Pombe
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi aliyotumwa na Chama
kuifanya ndani ya Serikali ameifanya vizuri sana tena kwa kasi kubwa katika
kipindi kifupi, tunataka sasa kasi hiyo ihamie ndani ya Chama, ili maadili
anayojenga kwa watumishi wa Umma, ayajenge pia ndani ya CCM Chama chenye
historia kubwa na jukumu zito katiaka ustawi wa Tanzania na watu wake.
Kazi
unayoifanya ndiyo hasa unayotakiwa kuwafanyia watanzania, wapo wengi ambao leo
hawakuelewi lakini kuna siku watakuelwa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema haya
yafuatayo katika kitabu chake cha Uogozi wetu na Hatma ya Tanzania, alisema -
“Hatuwezi
kujijengea utaratibu wowote ambao utazuia kabisa makosa yasifanyike hasa makosa
makubwa , lakini tunatazania kuwa yakifanyika wanaohusika watawajibika. Na
katika makosa makubwa ya maadili na utendaji mwenye jukumu la waziwazi la
kuwadhibiti wahusika ni Rais”
Mheshimiwa
Rais wetu anatimiza vyema jukumu hilo ambalo tangu mwaka 1994 wakati Mwalimu Nyerere
anaandika kijitabu hiki alijua kwamba hilo ni kjukumu la rais.
Ombi langu kwa
Wajembe wa mkutano Mkuu wa CCM, tumpe kura zetu za Ndio Rais Magufuli ili awe Mwenyekiti wa CCM.
Wito
wangu kwa Mwenykiti mpya Dr.Magufuli ni kwamba utakapochaguliwa katika kazi
zako za kwanza ndani ya Chama, napendekeza uanze na kuhakiki mali na
vitegauchumi vyote vya CCM. CCM ni chama tajiri sana lakini kuna baadhi ya
wanachama wenye nafasi katika Chama wanatumia majengo na mali nyingine za Chama
kama mali zao binafsi kwa faida yao na familia zao na sio kwa faida ya
wanachama wote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
0 comments:
Post a Comment