Mwaka
1994, Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere , aliandika kitabu
alichokiita Uongozi Wetu na Hatma ya
Tanzania. Wakati anaandika kitabu hiki, Taifa letu lilikua linakabiliwa na changamoto
kadhaa ambazo zilimfanya kuingilia kati akiwa na lengo la kutoa onyo , nasaha
na usia kwa watanzania , ikumbukwe kwamba wakati huo mwalimu alikua tayari ni
Rais mstaafu. Katika kitabu hiki mwalimu alitukumbusha kwamba Tanzania ni lulu
pekee kabisa katika historia ya Afrika. Nchi nyingine zote ni za kurithi kutoka
katika ukoloni. Nchi ya Tanzania iliundwa na sisi wenyewe kwa hiari yetu baada ya kuzikomboa nchi mbili tulizoziunganisha
yaani Tanganyika na Zanzibar.
Sisi
watanzania wote tunatakiawa kuitunza lulu hii, kwa kufanya kazi kwa bidii na
kufuata sheria za nchi kwaajili ya ustawi wetu na Taifa letu.
Mungu
ibariki Tanzania
0 comments:
Post a Comment