Baada
ya kimya kirefu tangu ashindwe kupata nafasi ya Urais nchini Marekani,
hatimaye aliyekuwa mgombea nafasi hiyo Hillary Clinton amejitokeza na
kudai kwamba ugomvi binafsi uliokuwepo kati yake na Rais Vladmir Putin
wa Urusi umechangia sana kumkosesha nafasi hiyo muhimu.
Clinton
ameeleza hayo wakati huu kukiwa na mzozo mpya kati ya serikali ya
Marekani na Urusi juu ya kuwepo taarifa za kiintelijensia kwamba Rais
Putin alidhamini kitengo cha udukuzi ili kiingilie na kuvuruga uchaguzi
mkuu wa nchi hiyo, na tayari Rais Obama ametoa agizo la kufanyika
uchunguzi na kusema kuwa serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya
Urusi.
Katika
mahajiano aliyofanya siku ya Alhamisi usiku, Clinton amesema kuwa Rais
Putin alikuwa akijaribu hata kuzivuruga kampeni zake ilimradi tu
kumharibia njia yake kutokana na “Ugomvi Binafsi.”
“Putin
alikuwa akinilaumu kwa kuwaambia ukweli raia wa Urusi kuwa
walidhulumiwa haki yao, vitu ambavyo vinafanana na kile alichoamua
kukifanya yeye kwa kuingia uchaguzi wetu na kuharibu kila kitu kama njia
ya kulipa kisasi,” amesema Hillary.
0 comments:
Post a Comment