Laws and regulations, politics and democracy in general

Vertical Sample

Saturday, December 17, 2016

MSUVA APIGA MAWILI, YANGA YAUA 3-0 SHAMBA LA BIBI

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM

Posted by Kurunzi za Siasa

YANGA imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 na  Simba iliyomalizia kileleni mzunguko wa kwanza kwa pointi zake 35. Lakini Simba inaweza kurejea kileleni kesho ikishinda dhidi ya wenyeji, Ndanda FC mjini Mtwara.
Shujaa wa Yanga leo alikuwa ni winga Simon Happygod Msuva aliyefunga mabao mawili kipindi cha pili baada ya kuseti moja kipindi cha kwanza.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Heri Sasii aliyesaidiwa na Hellen Mduma na Kassim Mpanga wote wa Dar es Salaam hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.

0 comments:

Post a Comment