Laws and regulations, politics and democracy in general

Vertical Sample

Thursday, August 30, 2018

TUJIFUNZE UTUMISHI WA UMMA KWA RAIS WETU DR. JOHN POMBE MAGUFULI

Na. Elias Magugudi,
Kurunzi la siasa

Natumaini viongozi wote hasa wateule wa Rais, wanatakiwa kujifunza utumishi wa UMMA kwa Rais wetu ambaye kiukweli anaishi katika maneno yake. Tusitumie nafasi zetu kwa kujipatia faida binafsi au kutafuta misaada ambayo haipo wazi eti kwa kisingizio cha watumishi mfano walimu na wengineo wengi.

Nampongeza sana Rais JPM katika suala la kodi analisimamia kwa dhati ya moyo wake. Nchi yetu imekua ikipoteza mapato mengi kwa njia za kihuni tu, tangu serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani mianya mingi imebanwa kila mtu anaishi kwa kazi halali na sasa hivi tunaheshimiana mtaani.

Tujifunze vizuri maadili ya utumishi wa umma ambayo kila mtumishi alikula kiapo cha kuyaishi na kulinda heshima ya utumishi wa umma.Tatakua tumewatumiakia vizuri Watanzania na sisi tutapata heshima mbele ya umma.

0 comments:

Post a Comment